Jumatatu , 9th Nov , 2020

Jumla ya watahiniwa 646,148 wamesajiliwa kufanya upimaji wa Kitaifa wa mitihani ya kidato cha pili kwa mwaka 2020, ambayo imeanza leo Novemba 9 Tanzania bara na itamalizika Novemba 20.

Wanafunzi wakiwa darasani, picha kutoka mtandaoni.

Kwa Mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Charles Msonde, akitangaza kukamilika kwa maandalizi ya mitihani hiyo, amesema kuwa kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 301,831 sawa na asilimia 46.71 na wasichana ni 344,317 sawa na asilimia 53.29. 

Dkt. Msonde, amewaonya wasimamizi wote pamoja na kamati zinazosimamia kuzuia mianya yoyote inayoweza kuharibu matokeo kutokana na udanganyifu, hivyo miongozo iliyotolewa Baraza la Mitihani izingatiwe ikiwemo watahiniwa wenye mahitaji maalum kupewa kipaumbele.

Baraza halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kujihusisha au kusababisha udanganyifu kutokea katika upimaji mitihani”, amesema Dkt. Msonde