Ijumaa , 16th Aug , 2019

Chama Cha ACT - Wazalendo kimebainisha kukamatwa kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ado Shaibu katika Makao Makuu ya chama hicho, Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa chama, Ado Shaibu amekamatwa akiwa anandaa mkutano wa kiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kwa ajili ya kuzungumza na waandishi habari.

Mpaka sasa polisi hawajasema sababu ya kutaka kuzuia mkutano huo na waandishi wa habari na taarifa ya chama imesema,"tunalitaka jeshi la Polisi lisimamie wajibu wake wa kulinda usalama na mali za raia badala ya kuwa sehemu ya chama dola, kwa kuvikandamiza vyama vingine vinavyotekeleza wajibu wao wa kisheria", imesema taarifa hiyo.

Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Kinondoni bado zinaendelea ili kufahamu sababu za kukamatwa kwa kiongozi huyo wa ACT - Wazalendo.