Jumapili , 27th Dec , 2020

Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla, pamoja na Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume ni miongoni mwa watumiaji wakubwa wa mtandao wa Twitter na huwa wanamijadala mbalimbali.

Hamisi Kigwangalla (kulia) na Fatma Karume (kushoto)

Baada ya muda mrefu Kigwangalla kuwa kimya kidogo kwenye mtandao huo, hivi karibuni alirejea na wafuasi wake wakampokea kwa furaha huku mmoja wa wafuasi hao akimkumbusha kuwa anaporejea ni lazima ajue Fatma Karume yupo anamsubiri.

Kigwangalla alimjibu kwa kushangaa kama Fatma maarufu Shangazi bado yupo na akahoji kama ataendelea kumsakama kama alivyokuwa anafanya wakati akiwa Waziri.

Lakini kwa upande wa pili Fatma Karume amejitokeza na kumjibu Kigwangalla kuwa yeye bado yupo na ataendelea kama ilivyokuwa zamani.