Jumapili , 26th Apr , 2015

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaongoza watanzania katika maadhimisho ya miaka 51 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifurahia jambo akiwa ameambatana na rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Ali Mohammed Shein.

Mara baada ya Kuingia uwanjani hapo Rais Kikwete amepigiwa mizinga 21 ya heshima pamoja na kukagua gwaride la vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama huku vikosi Mbalimbali vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ ,Jeshi la Polisi , Jeshi la Kujenga Taifa JKT pamoja na vya Jeshi la Magereza vikipita kwa ukakamavu katika sherehe hizo.

Sherehe hizo zimehudhuriwa pia na Rais wa Srikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ,Marais wastaafu wa Tanzania, viongozi mbalimbali wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na idadi kubwa ya wananchi ambao wamejitokeza kushuhudia sherehe hizo.

Shughuli nyingine zilizofanyika ni pamoja na ngoma za asili kutoka kwa makabila mbali mbali yaliyoipo nchini pamoja na onyesho maalumu la ndege za kivita zilizopita na kutoa heshima katika anga ya uwanja huo.