Jumanne , 7th Jan , 2020

Upelelezi wa kesi ya kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji MO, inayomkabili dereva taksi, Mousa Twaleb na wenzake watano raia wa kigeni ambao bado wanatafutwa, bado haujakamilika.

Pichani ni eneo la tukio alilotekwa MO Dewji.

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu, Wakili wa Serikali Faraji Nguka, amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba Mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine.

Watuhumiwa wengine ambao upande wa mashtaka inawatafuta ni raia wanne wa Msumbiji ambao ni Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issa Tomo, Zacarious Junior na mmoja wa Afrika Kusini, Phila Tshabalala, wanaodaiwa kumteka bilionea huyo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 21, 2020 itakapotajwa tena.

Mfanyabiashara Mohammed Dewji, alitekwa Oktoba 11, 2018 katika Hotel Colleseum iliyopo wilayani Kinondoni, na Oktoba 20, mwaka huo huo alipatikana maeneo ya viwanja vya Gymkana