Jumatatu , 27th Mar , 2023

Hali mbaya zaidi ya hewa inaweza kuwa njiani kuelekea jimbo la Mississippi nchini Marekani kufuatia vimbunga vilivyosababisha vifo vya watu 26, gavana wa  la Mississippi ameonya.

Gavana Tate Reeves alisema hatari kubwa bado ziko katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo.

Mamia ya watu wameyakimbia makazi yao kufuatia vimbunga vilivyosambaa katika miji ya Mississippi na Alabama siku ya Ijumaa usiku. Meya wa moja ya miji iliyoathirika zaidi alisema amepoteza marafiki wa karibu katika mkasa huo.

Kimbunga cha Ijumaa kilikuwa kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika jimbo la Mississippi katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja. Takriban watu 25 wamefariki katika jimbo hilo huku mtu mmoja akithibitishwa kufariki katika jimbo jirani la Alabama.

Miti imeng'olewa, malori yamepinduka kuwa nyumba na nyaya za umeme zimeshushwa na kimbunga hicho . Siku ya Jumamosi, manusura wa mkasa huo walionekana wakitembea huku na kule, wakiwa wamechanganyikiwa na kushtuka