Jumanne , 21st Feb , 2023

Zaidi ya watu 600,000 nchini Msumbiji huenda wakaathiriwa na kimbunga Freddy, ambacho kinatarajiwa kutua katika mikoa ya pwani wiki hii,

Mamlaka imesema kuwa  Maeneo yanayotajwa kuwa hatarini zaidi ni bonde la Zambezi, mikoa ya kati na kusini mwa jimbo la Inhambane.

Takriban watu 100,000 watahitaji msaada wa serikali iwapo kimbunga hicho kitaathirika kwa nguvu zote, kulingana na Agostinho Vilanculos, ambaye anaongoza idara ya rasilimali za maji.

Katika mkutano wa Kituo cha Kitaifa cha Operesheni za Dharura, afisa huyo  alielezea dhoruba ya kitropiki kama mfumo mkali wa hali ya hewa na upepo mkali wa kati ya kilomita 280   na kilomita 290 kwa saa.

Katika mji wa pwani wa Beira, wakaazi wamekuwa wakiimarisha nyumba zao kwa kutumia mifuko ya sandarusi na kuweka karatasi za chuma kwenye madirisha .

Pia wamekuwa wakihifadhi chakula na maji pamoja na vifaa vya mishumaa na taa.