Kingunge amkumbuka Lissu

Jumatatu , 8th Jan , 2018

Mwanasiasa mkongwe , Kingunge Ngombale Mwiru ambaye amelazwa katika hospitali ya Muhimbili kufuatia kung'atwa na mbwa amemkumbuka na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye amesafirishwa na kwenda Ubelgiji kwa matibabu zaidi. 

Kigunge amemjulia hali Tundu Lissu baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa akiwa amefuatana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati Kuu Mhe. Edward Lowassa walipomtembelea leo Januari 8, 2018 katika hospitali ya Muhumbili. 

"Vipi kuhusu Tundu Lissu? Nimeona mimi jinsi wanavyonifanyia hapa (madaktari) nimewauliza mimi tu niliyeng'atwa na mbwa mnanifanyia hivi Lissu mmemfanyaje maana majeraha yake yalikuwa makubwa" alihoji Kingunge 

Baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA kumueleza Mzee Kingunge juu ya hali ya Tundu Lissu kwa sasa ilimpa faraja mzee huyo na kusema kuwa 'Aluta Continua'