Ijumaa , 11th Dec , 2015

Mchakato wa kuwapata Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Ilala jana umeshindikana baada ya malalamiko kutoka kwa madiwani na wabunge wa vyama vya upinzani kudai kuhujumiwa.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bw, Mussa Natty

Katika halmshauri ya Kinondoni madiwani wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamedai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM), kilichomeka Mamluki kutoka Zanzibar kuelekea upigaji kura.

Wakitoa malalamiko yao baadhi ya Wabunge wa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuna hujuma ambayo inataka kufanyika kutokana na vyama vya upinzani kushikilizia viti vingi Jijini Dar es Salaam

Akizungumza mara baada ya Uchaguzi huo kuahirishwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bw, Mussa Natty amesema kuwa wanafuatilia masuala ya kisheria juu ya Wajumbe hao wanaolalamikiwa kisha watatolea maamuzi na kutaja tarehe nyingine ya Uchaguzi.

Wakati huo huo Uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Ilala nao uliingia Dosari na kuahirishwa ambapo upigaji wa kura utaendelea leo kutokana na mkanayingo wa jinsi ya upigaji kura huku vyama vya upinzani wakitaka uwe wa wazi na CCM wakitaka uwe wa siri.