Jumapili , 1st Mar , 2026

Kufuatia mfululizo wa majibizano ya mashambulizi kati ya mataifa ya Marekani na Israel dhidi ya Iran na Iran nayo kujibu, ripoti mbalimbali kutoka vyombo vya habari vya ndani vya Iran vimeripoti kifo cha kiongozi wa taifa hilo Ali Hosseini Khamenei.

Ni zaidi ya saa 23 sasa tangu Marekani iishambulie Iran na Iran kujibu kumekuwa na mfululizo wa kurushiana makombora huku athari mbalimbali zikitajwa kutokea ikiwemo kusitishwa kwa safari za anga kwenye anga la Nchi za Falme za Kirabu kutokana na Iran kurusha makombora katika nchi za Bahrain na maeneo mbalimbali ya UAE ikiwemo Dubai na Qatar, kwa lengo la kuvishambulia vituo vya kivita vya Marekani pamoja na Israel.

Mapema jana Jumamosi Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa wamefanikiwa kumuua Ali Hosseini Khamenei lakini taarifa hiyo haikuwa imethibitishwa wala kutangazwa na Iran.

Hata hivyo alfajiri hii ya Jumapili ripoti zimesambaa ikiwemo video fupi kutoka Iran zikieleza kuhusu Ali Hosseini Khamenei kuuawa mapema jana Jumamosi akiwa katika makazi yake huku pia wanafamilia wake na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Iran wakitajwa kufariki katika shambulio la Marekani na Israel katika makazi ya Khamenei huko Iran.

Kwa upande mwingine usiku wa Jumapili Machi 1, Iran inaelezwa kuushambulia mji wa Tel Aviv huko Israel wakilenga vituo muhimu vya kijeshi.