Jumatano , 12th Oct , 2016

Kipato cha wakulima nchini kinatarajiwa kuongezeka kupitia ukuaji wa sekta ya kilimo hasa baada ya makampuni makubwa ya uzalishaji mbolea duniani kuonesha nia ya kuja kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya kuzalisha mbolea hapa nchini.

Charles Mwijage

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema hayo leo wakati wa siku ya mwisho ya mkutano wa kimataifa wa kilimo cha kibiashara, uliokuwa unaangalia upatikanaji wa mbolea barani Afrika na kufanyika jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania ndio mwenyeji wa mkutano huo.

Mkutano huo umehusisha wasambazaji wa teknolojia mbalimbali za kilimo ikiwemo kampuni inayojihusisha na teknolojia ya uchambuzi wa sayansi ya udongo ambapo mkurugenzi wake Dkt. Edmund Matafu ameeleza uhusiano wa utengenezaji wa mbolea inayoendana na mahitaji ya udongo wa eneo husika.