Jumatatu , 25th Jul , 2022

Zaidi ya ndoa 365 zimevunjika katika Manispaa ya Temeke katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi sasa. Hayo yamebainishwa na Afisa ustawi wa Jamii wa manispaa hiyo Lilian Mafole na kusema chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hizo ni mifarakano, wivu wa mapenzi na kipato duni.

Watu wakivishana pete

Akizungumza na EATV Afisa Ustawi huyo amesema kutokana na ndoa hizo kuvunjika watoto wamekuwa wakiteseka kwa kukosa malezi na hatimaye watoto hao kujikuta wakifanyiwa ukatili wa kingono kutokana na kutokuwa na malezi bora kutoka kwa wazazi wa pande zote mbili.