Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kiwango cha udumavu nchini chashuka kwa asilimia 8

Jumatano , 20th Jul , 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya awamu ya tano itatoa msukumo mkubwa katika kukabiliana na tatizo la utapiamlo nchini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya awamu ya tano itatoa msukumo mkubwa katika kukabiliana na tatizo la utapiamlo nchini kwa kuweka mipango na mikakati imara ikiwemo kuongeza bajeti ya lishe, kuongeza virutubisho kwenye vyakula na kutumia vyema wataalamu wa lishe katika kupambana na tatizo hilo hapa nchini.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika hotuba yake ya uzinduzi wa Ripoti ya Dunia ya Utapiamlo ambayo imetilia mkazo masuala ya lishe kama msingi wa Maendeleo hapa nchini na Duniani kwa ujumla.

Makamu wa Rais amesema viongozi wa serikali katika ngazi zote za wilaya na mikoa wanatakiwa kuunga mkono jitihada za kuondoa utapimlo nchini kwa kuweka msukuko wa kipekee katika ngazi zote za maamuzi.

Ameeleza kuwa jitihada zinazofanywa na serikali kwa ushirikiano na wadau wa Maendeleo wa Ndani na Nje ya Nchi zimesaidia kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango cha udumavu nchini kutoka asilimia 42 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 34 mwaka 2015.

Amefafanua kuwa kutokana na mafanikio hayo, serikali imetoa mwongozo wa bajeti ya mwaka 2016/17 kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya masuala ya lishe kwa kila mtoto wa umri chini ya miaka mitano hapa nchini.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na fedha hiyo kuwa kidogo lakini serikali itaendelea kuongeza kiasi cha fedha kwenye bajeti zijazo hadi kufikia kiasi cha dola 8.5 sawa na shilingi elfu 18000 kwa kila mtoto hapa nchini kama ilivyoshauriwa na jopo la wataalamu wa Benki ya Dunia na wa masuala ya afya na uchumi duniani.

Makamu wa Rais pia ameziagiza Halmashauri zote Nchini kupitia TAMISEMI zihakikishe zinatumia fedha hizo vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa na sio vinginevyo.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya na Ustawi wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amemuahidi Makamu wa Rais kuwa Wizara yake itaendelea na jitihada zake za kuhakikisha malengo ya kuondoa utapimlo hapa nchini yanafikiwa kwa kuelimisha jamii namna ya kupambana na tatizo hilo.

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala