Jumatatu , 21st Dec , 2020

TAKUKURU mkoani Manyara, imefanikiwa kurejesha kiwanja ambacho ni mali ya  Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho kiliporwa na kuuzwa na Mwenyekiti wa CCM Kata, huku pia ikifanikiwa kurejesha zaidi ya Mil. 6 za mstaafu ambaye alitapeliwa.

Mkuu wa TAKUKURU wilayani Kiteto, Venance Sanga, (wa kwanza kushoto).

Akikabidi kiwanja hicho Mkuu wa TAKUKURU wilayani Kiteto, Venance Sanga, amesema kuwa kiwanja hicho kilitolewa na serikali ya Kijiji kwa matumizi ya chama  lakini kiongozi huyo alikihodhi na kukiuza kwa maslahi yake binafsi.

"Mwenyekiti wa CCM Kata hii alimega eneo hili, nusu akajenga nyumba yake na lililobaki akaliuza kwa shilingi laki 7, kwahiyo malalamiko yalikuwepo muda mrefu yakashindwa kuisha ndani ya chama", amesema Sanga.

Mbali na kuakabidhi kiwanja hicho pia, TAKUKURU wamefanikiwa kuokoa zaidi ya milioni sita za mstaafu Bakari Lugage, ambaye alitapeliwa na taasisi moja ya kifedha.