Jumatano , 19th Dec , 2018

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea amesema kuwa anaunga mkono jitihada zote zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea, akisalimiana na Rais Dkt. John Magufuli, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika upanuzi wa barabara ya Kimara hadi Kibaha kwa upana wa njia nane na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Kubenea amefunguka hayo wakati akitoa salam za wananchi wa Ubungo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika upanuzi wa barabara ya Kimara hadi Kibaha kwa upana wa njia nane.

"Mheshimiwa Rais, sisi juhudi zako zote za ujenzi wa Barabara na maendeleo mengine sisi tunaziunga mkono, lakini tunaomba uwaangalie wananchi waliobomolewa ili kupisha upanuzi wa barabara, wapatiwe fidia zao kwani maisha yao yamekuwa magumu sana", amesema Kubenea.

Rais Magufuli ameweka jiwe la Msingi la upanuzi wa barabara ya Kimara hadi Kibamba yenye urefu wa kilometa 19 ambapo viongozi mbalimbali walishiriki.