Jumatatu , 8th Aug , 2022

Mchunguzi lugha mwanadamizi kutoka Baraza la Kiswahi la Taifa (BAKITA) Musa Kaoneka, amesema kwamba neno la kumwagilia moyo lililoanzishwa na vijana amesema halina tofauti na kuupiga mwingi kwani ni aina ya misemo ya Kiswahi ambayo hayana shida.

Kiswahili

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na East Africa TV &Radio digital, na kutolea ufafanuzi wa neno kuumwagilia moyo likiwa na maana ya kwamba ni kujifurahisha na si lazima litumike kwenye unywaji wa piombe.

"Kwa sababu hilo neno limeanzishwa na vijana na mara nyingi tumezoea huwa wanaharibu lugha, kwahiyo wakianzisha tunaona kama wamekosea, kumwagilia moyo halina tofauti na kuupiga mwingi, ni maneno ya Kiswahili ambayo yanakua kama misemo ama nahau na kwenye Kiswahili hayana shjida," amesema Kaoneka