Jumanne , 3rd Dec , 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road nchini, Dkt Julius Mwaiselage, amesema Asilimia 99 ya wanawake wana uwezekano wa kupata Saratani ya matiti na asilimia moja ya wanaume wanauwezo wa kupata Saratani ya aina hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road nchini, Dkt Julius Mwaiselage.

Dkt Mwaiselage ametoa kauli hiyo leo Desemba 3, 2019, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreaskFast cha East Africa Radio, kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 12 Asubuhi hadi saa 4 kamili wakati akizungumzia hali ya ugonjwa huo hapa nchini.

"Chanzo kikubwa cha Saratani ya matiti ni mwanamke anapokuwa na kichocheo cha hali ya juu ndiyo huchangia wanawake kupata Kansa, ninaposema kichocheo huwa namaanisha Homoni" amesema Dkt Mwaiselage.

Jana Desemba 2, 2019, wakati akizungumzia mafanikio katika kipindi cha miaka 4, Mwaiselage amesema taasisi hiyo imefanikiwa kuwatibu wagonjwa wa saratani zaidi ya 6400.