Alhamisi , 30th Jun , 2022

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, leo Juni 30, 2022 ameshiriki zoezi la  kuaga kundi la tatu la Kaya zaidi ya 25 za wananchi wanaohama kwa hiari yao kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Handeni mkoani Tanga.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, akiagana na wananchi Ngorongoro

Wananchi hao ni wale waliokuwa wakiishi ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambao wameamua kuhama kwa hiari yao kuelekea Kijiji cha Msomera ili kupisha shughuli za uhifadhi.

Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana amewaaga  wananchi hao akiwa na viongozi wa kamati ya amani na maridhiano nchini inayoundwa na viongozi wa dini pamoja na uongozi wa mkoa wa Arusha na kuwahakikishia kuwa serikali chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, imewaandalia mazingira mazuri na salama katika Kijiji cha Msomera.