
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amesema lengo ni kuwadhibiti matapeli wa mitandaoni
Aidha Waziri NAPE amesema serikali imeteua kamati ya watu tisa watakaokuwa na jukumu la kutathimini uchumi wa wanahabari.
Waziri Nape amewataka watanzania kuhakiki laini zao kwa kuwa yoyote aliyesajili kwa uongo hawezi kuhakiki laini hiyo
"Kuna laini nyingi mtaani, ambazo watu wametumia vitambulisho vya watu wengine kusajili laini, na zinatumika kufanya utapeli, kwa hiyo laini tunazokwenda kuzizima ni zile ambazo zimesajiliwa, lakini zimesajiliwa kwa uongo,"
"Kama hujaisajili kwa uongo nenda kaihakiki, yoyote aliyesajili kwa uongo hawezi kuhakiki, kwa sababu ule utaratibu wa uhakiki utamnyima baadhi ya taarifa" amesema Waziri Nape