Jumanne , 11th Aug , 2020

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini nchini (LATRA) imewataka wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuweka utaratibu sahihi utakaosaidia kuondoa usumbufu kwa abiria wao pamoja na wamiliki.

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini nchini (LATRA) imewataka wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuweka utaratibu sahihi utakaosaidia kuondoa usumbufu kwa abiria wao pamoja na wamiliki.

Akizungumza na EATV Meneja Leseni Barabara (LATRA) Leo Ngowi amesema hatua hiyo inakuja baada ya kuanzishwa mfumo wa ukataji wa tiketi kwa njia ya mtandao ambao unalengo la kuondoa upotevu wa mapato kwa wasafirishaji pamoja na kuondoa mlolongo wa kufuata tiketi katika vituo vya mabasi.

Ngowi amesema kuwa baada ya utafiti wa muda mrefu walibaini kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa abiria, kuongeza kuwa kwa sasa mfumo huo utasaidia upatikanaji wa taarifa muhimu ikiwemo kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali na kuwezesha wasafirishaji kukopesheka kutokana na taarifa za miamala hivyo kuongeza uwekezaji.

"Abiria anapotaka kusafiri anaingia kwenye vituo vikubwa vya mabasi na mara nyingi kumekuwa na kero nyingi ikiwemo wamiliki kupoteza fedha ndyingi kwahiyo kwa kutumia mfumo huu hilo tatizo halitakuwepo na lingine ni kuweka takwimu sahihi ya idadi ya mabasi na mapato yanayopatikana" amesema Ngowi