Alhamisi , 24th Mar , 2016

Rais Mteule wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuapishwa muda mfupi ujao katika uwanja wa Amani mjini Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza leo kuwa ni siku ya mapumziko ili kuwawezesha watu wengi zaidi kuhudhuria sherehe hiyo muhimu katika visiwa vya Zanzibar.

Miongoni mwa watakaohudhuria ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa viongozi mbalimbali wa Zanzibar na viongozi wastaafu wa kitaifa.

Uwanja wa Amani kwa sasa umefuriika mamia ya wananchi wakiangalia gwaride na viongozi mbalimbali wa kitaifa ambao wanaingia kushiriki zoezi hilo muhimu.

Rais Mteule Dkt. Ali Mohamed Shein alitangazwa juzi na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salum Jecha kwa ushindi wa asilimia 91.4% na kuwashinda wagombea wengine 13.