
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga akisoma tamko lao.
Tamko hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga ambapo wameitaka EWURA kusitisha kusudio lao hilo la maoni ya kuiongezea muda kampuni hiyo mpaka serikali itakapotekeleza mapekendezo yaliyotolewa na bunge la Tanzania mwaka 2014 kuhusu na sakata la uchotwaji wa mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.
Kwa upande wake meneja mawasiliano na uhusiano Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Maji nchini(EWURA) Titus Kaguo amesema kinachoendelea kwa sasa ni uwasilishaji wa maoni hivyo kwa yeyote mwenye wasiwasi na ushahidi wa lalamiko lake apeleke maoni yake EWURA kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Maji nchini(EWURA) Titus Kaguo akifafanua jambo.