Jumatano , 9th Sep , 2015

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimekemea kauli zenye kuwajengea hofu wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia unaoendelea kwa kutoa mifano isiyoshabihiana na hali iliyopo nchini ikiwemo kufananisha na nchi zenye machafuko

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk.Helen Kijo-Bisimba

Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari imemtaka mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Mh. John Magufuli kufuta kauli zake ikiwemo ya kufanisha mchakato wa uchaguzi na vuguvugu la mabadiliko ya Libya pamoja na serikali yake kuwapiga risasi wahalifu wa kutumia silaha.

Mh. Magufuli mnamo tar 28 Agost akiwahutubia wakazi wa Mbalizi Mbeya vijijini alisema “Msitoe hukumu ya jumla zipo nchi zilifanya hivyo zilijuta,Libya ya Gadafi ilikuwa ukioa unapewa nyumba, unatafutiwa mtaji ,elimu na umeme bure lakini wananchi walichoka raha.....wakasema wanaondoka lakini wale vijana waliosema wanataka raha na wale vijana waliosema wanataka ukombozi wa haraka ndio wa kwanza kuvuka bahari ya Mediteranian kwenda Ulaya."

Kituo hicho kimesema kauli hizo zinatoa vitisho kwa wapiga kura kinyume na demokrasia kwa kuwa huwezi kufananisha mabadiliko ya kimapinduzi ya Libya na umwagaji damu uliotokea huko na mabadiliko ya amani kwa kupitia mchakato wa uchaguzi za kidemokrasia.

Taarifa hiyo imeogeza kuwa kauli hizo za mgombea huyo ni za kukemewa kwa kuzingatia nchi na chaguzi zinaongozwaq kikatiba na Katiba inakinzana kabisa na kauli zilizotolewa na kiongozi huyo