
Mgombea urais kupitia CUF Profesa Ibrahim Lipumba
Profesa Lipumba, amesema mradi wa kufua umeme kwa kutumia makaa ya mawe ya Kiwira ni mradi ambao hauchukui muda mrefu, hivyo serikali ingeweza kuongeza upatikanaji wa umeme nchi mzima kwa kutumia makaa ya mawe ya Kiwila.
Ameongeza kuwa mradi huo wa umeme ungeweza kusaidia kwa haraka wakati serikali inajipanga kupata fedha za kukamilisha mradi wa Bwawa la Nyerere, kwani mradi huo umeanzishwa kwanza badala ya kutekelezwa kwanza.
''Wakati tunajipanga vizuri kupata fedha za kukamilisha mradi wa stiegler's Gorge, haya ni mapungufu ya serikali ya CCM, hakuna sababu kwanini ule mradi wa kufua umeme wa megawatt 200 mpaka 300 kwa kutumia makaa ya mawe ya Kiwila mpaka hivi sasa bado haujatekelezwa", amesema Profesa Lipumba.