Jumatatu , 21st Jan , 2019

Baada ya Spika Job Ndugai hivi karibuni kumtaka Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Aniphas Lissu kurejea nchini kwakuwa hana kibali cha kuzuruua huko Ulaya, mbunge huyo amemjibu Spika akidai amejuaje kama amepona ilhali hajawahi kumjulia hali kwa simu.

Mbunge wa Singida Mashariki

Lissu ambaye alipelekwa nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya matibabu yale aliyoyapta nchini Kenya baada ya kushambvuliwa kwa risasi zaidi ya 30 amesema kwamba Spika Ndugai hajui chochote kwasababu hajataka kujua tofauti na watu wengine ambao wanamtafuta na kumjulia hali.

Akifanya mahojiano na gazeti la kila siku la Tanzania, Lissu amesema kwamba, "Spika Ndugai hajui chochote, hajui nimepona au sijapona. Hajui kwa sababu hajataka kujua, hajataka kunipigia simu kuniuliza kama ambavyo wengine wananipigia simu. Hajataka kuwasiliana na familia yangu, hajui kwa sababu ametaka kubaki asiyejua"

“Spika anajuaje kwamba nimepona?. Anajua masharti niliyopewa na daktari ni yapi?. Anajua nimetokaje hospitalini?”, amehoji Tundu Lissu.

Juma lililoisha, Spika wa Bunge, Job Ndugai alimtaka Mbunge huyo wa Singida Mashariki (CHADEMA), kurejea nyumbani kwa kuwa hana kibali cha kuwa nje ya nchi huku akiongeza kwamba hawezi kumpangia Lissu mambo ya kusema ila ajue hana kibali cha kuendelea kuwa nje ya nchi wakati ofisi ya Spika haina taarifa.