Lukuvi amsimamisha kazi Mkurugenzi

Jumamosi , 16th Dec , 2017

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi amemsimamisha  kazi Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba  NHC Bw. Nehemia Mchechu kupisha uchunguzi.

Katika taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa wizara ya ardhi Doroth Mwanyika imebainisha kumsimamisha Mchechu  kwa mamlaka aliyopewa waziri Lukuvi kupitia kifungu f. 35 cha kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2009.

Waziri Lukuvi pia  ametoa agizo kwa bodi ya Shirika hilo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa huduma za mikoa na Utawala Raymond Mndolwa ili kupisha uchunguizi wa tuhuma zinazowakabili watendaji hao.