Alhamisi , 11th Aug , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba tayari ameshamkabidhi fimbo Waziri wa zamani wa Ardhi William Lukuvi, kwa ajili ya kuwachapua mawaziri vijana na ndiyo maana wanachapa kazi ipasavyo.

William Lukuvi

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 11, 2022, wakati akiingia mkoani Iringa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika maeneo mbalimbali ya nchi.

"Mmewaona mawaziri hakuna aliyezidi miaka 56 hawa wote nimemkabidhi fimbo Lukuvi wakifanya vituko anawachapua, tungeweka mibaba mikubwa mikubwa angeshindwa kuwachapua angewatizama wanaongea lugha moja na kusema bwana usifanye hivyo," amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia ameongeza, "Lakini hawa (Mawaziri waliopo sasa) ni kuwachapua kwenda mbele, ndiyo maana vinakwenda mbio kweli kweli kufanya kazi,"