
Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) akipokea fomu.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Agosti 26, 2020 ilianza kutoa fomu za kugombea urais wa visiwa hivyo yakiwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, huku mgombea wa chama tawala (CCM), Hussein Mwinyi, akiwa wa kwanza kujitokeza ambapo zoezi hilo litaendelea hadi Septemba 9, 2020.
Mgombea wa kwanza kuwasili kwenye ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) asubuhi ya Jumatano alikuwa Hussein Mwinyi wa chama tawala cha Mapinduzi (CCM), ambaye alifuatiwa na mwenzake wa chama cha Wakulima (AFP), Said Soud.
Akitoa fomu hizo na kueleza masharti yanayopaswa kuzingatiwa na wagombea hao, Mwenyekiti wa ZEC Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud alisema wagombea hao sasa walikuwa na dhima ya kusaka wadhamini na kurejesha fomu hizo baadaye kwa uhakiki.