Jumatatu , 26th Jul , 2021

Rais wa Tunisia Kais Saied amemfukuza kazi Waziri Mkuu Hichem Mechichi na kusitisha bunge, kufuatia ghasia kali zilizoibuka katika maeneo yote ya nchi hiyo.

Rais wa Tunisia Kais Saied (Kushoto) na Kulia ni wananchi wakisherehekea mara baada ya maamuzi ya Rais kumfuta kazi Waziri Mkuu na Bunge kusitishwa nchini Tunisia.

Maelfu ya waandamanaji, wamekasirishwa na jinsi serikali inavyoshughulikia Covid-19 walivamia mitaani na kupambana na polisi siku ya jumapili.

Rais Kais Saied amesema atasimamia suala la kukabiliana na Covid-19 akisaidiwa na Waziri Mkuu mpya, na kusema analengo la kutuliza hali ya nchi.

Hata hivyo wapinzani wa Rais Saied, wamezifananisha hatua alizochukua sawa na mapinduzi.