Jumamosi , 28th Aug , 2021

Wasichana 11 waliokatisha masomo yao kutokana na kubeba ujauzito katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, wamepatiwa vifaa vya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi ikiwemo vyerehani na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini (SIDO).

Baahi ya mabinti waliokatisha masomo baada ya kupata ujauzito mkoani Simiyu

Akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo ya ujasiriamali kwa mabinti hao waliopata ujauzito wangali masomoni yaliyowezeshwa na Shirika la Restless Development, Meneja wa SIDO mkoa wa Simiyu, Athanas Moshi, amesema wameamua kutoa vyerehani hivyo kwa mabinti hao ili kuwa mwanga wa kiuchumi katika maisha yao na watoto wao.

Kwa upande wao, mabinti hao kupitia risala lao wamesema msaada huo wa vyerehani waliopewa na Shirika la SIDO watautumia vizuri katika suala zima la uzalishaji mali, ingawaje wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mitaji.