Jumatatu , 27th Jun , 2016

Wakazi wa eneo la Kinondo ya Mabwepande, jijini Dar es Salaam, wamemuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kufika katika eneo lao ili kutatua mgogoro wa ardhi uliopo baina yao na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.

Wananchi hao wamesema hayo katika Mkutano na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi aliefika katika eneo hilo ili kutatua mgogoro huo ambapo umedumu kwa kipindi kirefu.

Aidha, Wananchi hao wameongeza kuwa wanakosa sehemu ya kufanyia shughuli za kawaida pamoja na makazi kutokana na eneo kubwa hilo kushikiliwa na mwekezaji huo bila kufanyia muendelezo wowote.

Akiongea na Wananchi hao Mkuu wa wilaya ya Kinondoni amewakikishia wakazi hao kumfikisha hapo Waziri wa Ardhi katika eneo hilo ili kutatua mgogoro huo na kuwataka wawe na subira wakati suala lao linashughulikiwa.