Jumapili , 16th Feb , 2020

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla, ameandika kuwa mara nyingi tabasamu la mtu hutokea mara baada ya kupitia machozi, jasho na damu nyingi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla.

Waziri Kigwangalla ameyaandika hayo leo Februari 16, 2020 kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Tabasamu la namna hii, toka kwa mtu mwenye mvi kama mimi, huja baada ya machozi mengi, jasho na damu! Hizi mbili hazishabihiani, lakini zote za tabasamu, shangwe, nderemo na vifijo na zile za machozi, jasho na damu, zina maana kubwa sana kwenye maisha ya mwanadamu" ameandika Waziri Kigwangalla. 

Ikumbukwe miezi kadhaa nyuma, Waziri Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Twitter, aliandika kuhusu uwepo wa watu wanaotamani atumbuliwe katika nafasi yake ya Uwaziri, na wengine wakimuwinda kutaka kutoa roho yake.