Alhamisi , 21st Oct , 2021

Watu wanaopenda kusafiri na kurudi makwao hususani katika kipindi cha likizo za mwisho wa mwaka, wametakiwa kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa magari yao ipasavyo na kwa wale ambao hawajawahi kuendesha magari umbali mrefu basi wakodi madereva kwa usalama wao.

CEO wa Mac Auto Express Garage, Edwin Temba

Ushauri huo umetolewa  leo Oktoba 21, 2021, na CEO wa Mac Auto Express Garage, Edwin Temba, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, alipokuwa akizungumzia mambo muhimu kwa wale wanaopenda kundesha magari yao wao wenyewe.

"Kama una leseni na umeshazoea kuendesha gari kutoka Mbezi hadi mjini, hujawahi kuendesha gari kutoka Dar hadi Mbeya, mwezi Desemba tafuta dereva mlipe akupeleke unakoenda wewe na familia yako," amesema Temba.

Aidha, Temba ameongeza pia, "Wakati wa kusafiri watu wengi huwa hawafanyi ukaguzi na wasichokijua kuna utofauti wakati unaagiza gari Japan wao ni baridi hivyo wanatumia tairi za waya, sisi Dar ni joto tunatumia tairi ya nyuzi, hivyo tairi ya waya ukiiendesha kutoka Dar hadi Moshi ina-over heat na lami yetu ina joto hivyo lazima itapasuka”