Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego
Awali wajumbe wa kikao hicho wakiwamo Diwani wa Likombe Mukhsin Komba alionekana kushinikiza kuondolewa kwa Meya huyo na kuungwa mkono na Naibu Meya ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, Erick Mkapa.
Mwanasheria wa Manispaa hiyo, Sifaeli Kulanga, amepingana na matakwa ya wajumbe hao kwa madai kuwa yanakwenda kinyume na taarifa ya tume iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara kuchunguza tuhuma zinazomkabili Meya huyo, ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya fedha.
Baada ya mijadala hiyo baina ya wajumbe na mwanasheria akiungwa mkono na mkurugenzi wa manispaa Beatrice Diminic, Naibu Meya Erick Mkapa akawasihi wajumbe waridhie hoja za mwanasheria, huku Meya akishukuru kutokana na maamuzi ya kumuacha katika nafasi yake.



