Jumanne , 19th Aug , 2025

Wakati Marekani ikianzisha operesheni kubwa ya kupambana na dawa za kulevya katika visiwa vya Caribbean, Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametangaza kutumwa kwa wanamgambo milioni 4.5 nchini humo. 

Washington hivi majuzi iliongeza maradufu zawadi ya kukamatwa kwa Maduro hadi dola milioni 50, akishutumiwa kuwa sehemu ya makundi yanayofanya biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Nicolas Maduro ametangaza kwenye televisheni ya taifa kwamba Wanamgambo waliotayarishwa, walioamilishwa na wenye silaha wako tayari,

Kundi la wanamgambo wa Venezuela lililoasisiwa na Hayati Rais Hugo Chavez, ambaye Maduro alimrithi, kwa mujibu wa vyanzo rasmi, wanajumuisha takriban watu milioni 5, raia na askari wa akiba, na wako chini ya uongozi wa jeshi.