Jumatano , 21st Sep , 2022

Mamlaka nchini Nigeria  zinasema kwamba zaidi ya watu  300 wamepoteza maisha huku wengine zadi ya 100,000 wakiwa hawana mahali pa kuishi kutokana na mafuriko makubwa nchini humo tangu  mwezi  Julai mwaka huu. 

Makazi ya watu na mashamba vimeharibiwa vibaya katika Taifa hilo la Magharibi mwa Afrika ambalo limekumbana na janga baya kabisa la mafuriko kuwahi kutokea kwa miaka mingi iliyopita.  

Mamlaka zinasema kwamba majimbo 29 kati ya 36 yameathiriwa vibaya na mafuriko hayo  ambayo yamesababishwa na  mvua kali zilizoisababisha mabwawa makubwa kufurika na kupelekea maji kufika mpaka nchi jiani ya   Cameroon. 

Mito pia na yenyewe imefurika maji mengi.  Kitengo cha dharura nchini humo kimeonya kwamba marufiko zaidi yanatarajiwa kutokea ndani ya siku zijazo. Serikali imetakiwa kuwaondoa watu kutoka kwenye maeneo ambayo yapo hatarini kukubwa na mafuriko hayo.