Alhamisi , 29th Oct , 2020

Aliyekua Mbunge wa Jimbo la Hai ambae pia ni Mwenyekiti wa chama Kikuu cha Upinzani, lakini pia alikua Kiongozi Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani, Freeman Aikael Mbowe, ameshindwa kutetea kiti chake katika Jimbo hilo baada ya kuangushwa na mpinzani wake wa karibu, Saashisha Mafuwe wa Chama

Kulia ni Freeman Mbowe aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Hai, Kushoto ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Hai, Saasisha Mafuwe.

 cha Mapunduzi (CCM).

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Hai, Yohana Elisha Sentoo, amemtangaza Saashisha Mafuwe kupitia Chama Cha Mapinduzi, (CCM),kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya ubunge wa jimbo la Hai ambapo amepata kura 89,786 huku Freeman Mbowe wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA), akipata kura 27,684.

Jimbo la Hai ni miongoni mwa majimbo ambayo yamefuatiliwa kwa ukaribu sana katika kipindi chote cha kampeni, uchaguzi na hata wakati huu wa matokeo na hii ni kutokana na kuwa jimbo hilo kwa miaka mingi limekuwa ngome ya chama kikuu cha upinzani (CHADEMA), zaidi likiongozwa na Mwenyekiti Taifa wa chama hicho ambaye pia alikuwa mgombea.

Mbowe ameliongoza jimbo la Hai tangu mwaka 2000, baadaye mwaka 2005 aligombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, 2010 alirejea tena kugombea ubunge wa jimbo hilo na kuibuka msihindi huku akiendelea kuwa Mbunge hadi mwaka 2020.