Ijumaa , 13th Nov , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Magufuli Dkt. John Magufuli, ameteua mawaziri wawili katika Baraza Jipya la Mawaziri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Magufuli Dkt. John Magufuli

Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango. 

Dkt. Philip Mpango

Rais Dkt. Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Prof. Palamagamba Kabudi

Mawaziri hao walikuwa wakishika nafasi hizo katika Baraza lililopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Uteuzi huo umeanza leo Novemba 13, 2020.