Jumatano , 5th Aug , 2020

Mahakama ya rufaa Tanzania imetengua uamuzi wa awali wa mahakama kuu na kusema makosa yaliyochini ya kifungu cha 148 (5) ya CPA mfano Makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha yaendelee kuwa hayana dhamana.

Mahakama ya rufaa Tanzania imetengua uamuzi wa awali wa mahakama kuu na kusema makosa yaliyochini ya kifungu cha 148 (5) ya CPA mfano Makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha yaendelee kuwa hayana dhamana.

Hukumu hiyo hii leo imesomwa na msajili wa mahakama ya Rufani Eva Nkya ambaye amesema Katiba na wajibu wa serikali ni kulinda haki ya kila mwananchi ufafanuzi uliotolewa kwa kina na wakili mkuu wa serikali Gabriel Malata.

Rufaa hii ilikuwa inapinga uamuzi wa Mahakama kwenye Shauri la Madai Namba 08 la 2019 ambapo Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Dar es Salaam ilimpatia ushindi Bw. Sanga mnamo Tarehe 18 Mei 2020. 

Mahakama Kuu iliiagiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurekebisha kifungu hicho ndani ya miezi 18 kutoka siku ya kutolewa kwa hukumu huku ikiionya Jamhuri kuwa kushindwa kufanya hivyo kutasababishwa kufutwa.

Awali kesi hiyo ilikuwa ikisimamiwa na mawakili wa utetezi watatu akiwemo Jebra kambole,Mpate Mpoki Jonathan Mbuga Ambapo wamesema bado Kuna vifungu katiba katiba ya nchi ambavyo ni kandamizi.

Kwa Upande wake mtendaji Mkuu Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu wa Tanzania (THRDC) Onesmo Ole Ngurumwa ametoa wito kwa Watetezi wa Haki za kuendelea kupigania vifungu vinavyokiuka haki

Rufaa hii inapinga uamuzi wa Mahakama kwenye Shauri la Madai Namba 08 la 2019 ambapo Mahakama Kuu ya Tanzania; Masjala ya Dar es Salaam ilimpatia ushindi Bw. Sanga mnamo Tarehe 18 Mei 2020 huku ikitangaza kuwa kifungu cha 148(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, 1985 kinakinzana na Ibara ya 13(3), 15(1) na 2(a) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo Mahakama Kuu iliiagiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurekebisha kifungu hicho ndani ya miezi 18 kutoka siku ya kutolewa kwa hukumu huku ikiionya Jamhuri kuwa kushindwa kufanya hivyo kutasababishwa kufutwa.