Jumatano , 15th Oct , 2025

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Oktoba 15, 2025 mbele ya mahakama hiyo na kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo Jaji Fredrick Manyanda

Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma imetupilia mbali kesi ya Luhaga Mpina na ACT-Wazalendo, waliokuwa wakipinga kuenguliwa kwa Luhaga Mpina katika nafasi ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kupitia chama hicho.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Oktoba 15, 2025 mbele ya mahakama hiyo na kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo Jaji Fredrick Manyanda ambapo mahakama imesema kuwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) haipaswi kuingiliwa na chombo chochote kwa jambo ambalo ilifanya kwa nia njema.

Kwa uamuzi huo, Mpina hataweza kushiriki kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wakati vyama vingine vya siasa vinavyoshiriki vikiendelea na kampeni.

Majaji wengine waliosikiliza kesi hiyo ni Sylvester Kainda na Abdallah Gonzi