Jumatatu , 18th Feb , 2019

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, leo Februari 18, 2019, imetengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF) wa kambi ya mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wale wa Maalim Seif.

Profesa Lipumba akiwa akiwa na Maalim Seif.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Dk. Benhajj Masoud ambapo baada ya kubatilisha uteuzi wao, amesema majina yaliyokuwa yamependekezwa na kambi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, hawakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa bodi hiyo, hivyo nao hawakuwa wamekidhi matakwa ya sheria.

Wakili Juma Nassoro wa CUF kutoka kambi ya Maalim Seif,  amesema wajumbe wa bodi waliokuwepo wanaendelea na majukumu yao licha ya kwamba muda wao umeshaisha, hadi hapo wajumbe wengine watakapoteuliwa.

Katika kesi ya Msingi, Mbunge wa Malindi (CUF), Ally Saleh,  alifungua kesi hiyo akipinga uamuzi wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita) wa kuwaidhinisha wajumbe waliopendekezwa na kambi ya Profesa Lipumba kuwa wajumbe wapya wa bodi hiyo.