Alhamisi , 16th Dec , 2021

Mahakama ya wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha maisha jela George Lupindu (19) mkazi wa kijiji cha Ngalawale kwa kosa la kumbaka mtoto wakike mwenye umri wa miaka 9.

Akisomewa hukumu hiyo  na hakimu Isaack Ayengo katika shauri namba 37/2021 Geaorge Lupindu ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 130(1)(2)(e) na 131(3) cha Kanuni ya Adhabu, Sura namba 16 ya Sheria za Tanzania kama ilivyofanyiwa Mapitio  mwaka 2019.

Imeelezwa na Mwendesha Mashtaka Asifiwe Asigile kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Julai 7 mwaka huu ambapo anadaiwa kumrubuni mtoto huyo (jina limehifadhiwa) wakati akitokea shuleni kwa kumdanganya kuwa anampeleka nyumbani kwao na kisha kumtenda unyama mtoto huyo.