Jumamosi , 16th Jul , 2016

Majaji ambao wanasimamia shindano la Dance100% 2016 wamewataka vijana kuchangamkia nafasi ya bure ya shindano hilo kuonyesha vipaji vyao ili waweze kutambulika kupitia sanaa ya kucheza ambayo ni ajira kubwa kwa sasa nchini na nje ya nchi.

Majaji wa shindano la Dance100% 2016 walipokuwa kazini Leaders Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na EATV wakati wa ufunguzi wa shindano hilo ambalo umeanza leo jijini Dar es salaam katika viwanja vya Leaders Club Jaji wa miaka mingi katika shindano hilo Bwn. Super Nyamwela amewataka vijana kuhakikisha wanajipanga vilivyo kwani wengi wamepania sana kuonyesha vipaji vyao kupitia shindano hilo.

‘’ Mimi huwa natoa alama kulingana na jinsi ambavyo kundi huonyesha uwezo wa kucheza na huwa sioni aibu kutoa alama ndiyo maana utaona kuna kundi naweza kutoa alama 8 na linguine 90 hivyo vijana wasiogope wajitume watafanikiwa zaidi’’ Amesema Jaji Nyamwela.

Kwa upande wake Jaji Lotus amesema vijana wanatakiwa kutambua umuhimu wa shindano hilo kwao kwa kuwa licha ya zawadi watu wengi hasa bendi na wanamuziki binafsi huchukua vijana kutoka katika shindano hilo na kuwasihi ambao wamekosa leo kuweza kujitokeza katika usaili mwingine jumamosi ijayo

Hata hivyo Jaji wa tatu katika mashindano hayo Khalila amewataka mabinti kujitokeza kwa wingi kwani tasnia ya muziki kwa sasa inawahitaji wengi zaidi na kuwaomba wazazi kuweza kutoa nafasi kwa vijana wao kushiriki shindano hilo.
Shindano hili limedhaminiwa na Vodacom na Coca-Cola litakuwa linarushwa kila siku ya Jumapili saa moja jioni EATV.

Makundi matano yaliyoingia tano bora hapa Leaders Club ni Mafia Crew, The DDI Crew, BBK BBoys, Mazabe Powder, Tatanisha Crew

Tags: