Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Majaji waicharukia serikali kesi ya Lema

Jumatatu , 27th Feb , 2017

Mwenyekiti wa kikao cha jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, kinachoendelea Arusha, Bernard Luanda, leo amegeuka mbogo kwa wanasheria wa serikali kwa kitendo cha kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhamana kwa lengo la kumyima haki.

Lema akirudishwa gerezani (Picha: Maktaba)

Akizungumza Mahakamani hapo leo mbele ya majaji wenzake Stella Mugasha na Jaji Kipenka Mussa, Luanda amesema haipendezi na haingii akilini mtu (Lema) kushikiliwa kwa miezi mine bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki.

“Tunaomba ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikai (DPP) muwe makini sana maana mnatufanya wanasheria wote hatuna akili na mnachafua Mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo na imetushitua sana,” alisema huku akishauriana na wenzake mara kwa mara kwa masikitiko.

Aliendelea kusema kuwa ofisi ya DPP inaitia najisi taaluma hiyo, kitu kipo wazi ila wanafanya vitu vya ajabu na havipendezi.

Alihoji jaji Luanda kuwa “Tumesoma faili lote tunashangaa hivi kweli ofisi ya mwanasheria mkuu ina wanasheria kweli na kama wapo kwa nini huyu mtu (Lema) awe ndani mpaka leo?”.

Alisema kwa kuwa mikono yao kisheria imefungwa hawawezi kufanya chochote kwa leo na kuwataka Mawakili upande wa Lema kurudi Mahakama Kuu, kuendelea na maamuzi ya dhamana.

Godbless Lema

Hali hiyo ilitokana na Wakili wa serikali Faraja Nchimbi kusimama mahakamani hapo na kuomba kuiondoa rufaa hiyo kwa madai kuwa ipo nje ya uwezo wake.

“Waheshimiwa Majaji baada ya timu yetu ya wanasheria kupitia kwa kina rufaa hii kwa sababu zisizozuilika tumeona hatupo tayari kuendelea na rufaa hii, maana hatukupeleka kusudio (Notisi) kwa msajili muda ulipita, hivyo tunaomba kuiondoa na uamuzi wa kuiondoa rufaa hii tumeufikia Ijumaa muda uliisha kuja mahakamani,”. Alisema Nchimbi.

Baada ya kuwasilisha ombi hilo, Wakili wa Lema Peter Kibatala, alisimama na kusema upande wao hawana pingamizi ila waliomba hoja za awali za rufaa hiyo ziondolewe Mahakamani hapo bila kunakiliwa.

Baada ya ombi hilo Jaji Kipenka Mussa alipokea kwa niaba ya Majaji wenzake na kukubali ombi la kuiondoa rufaa hiyo namba 9/2017.

Wakili Peter Kibatala

Aidha Jaji Luanda alimkaribisha jaji Stella Mugasha pia kuongea kwa niaba yao ambapo alisema mahakama imekubali ombi la pili la kuiondoa rufaa namba 10/2017, baada ya Wakili Paul Kadushi kuomba kuiondoa pia.

Wakili wa Lema Peter Kibatala, alilazimika kusimama tena Mahakamani hapo kusema kuwa upande wao unasikitika kuona ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP wanatumia Mahakama kwa njia ya kumnyima haki mteja wao, hivyo aliomba mahakama hiyo iwatatulie tatizo la kisheria lililojitokeza hadi mteja wao awe ndani hadi sasa.

Kibatala aliongea hayo huku akishindwa kujizuia na kumwaga chozi la huzuni mahakamani hapo mbele ya Majaji hao.

 

HABARI ZAIDI

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria