Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Majaliwa atoa maagizo kwa viongozi CCM

Jumapili , 17th Feb , 2019

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Mkoa na Wilaya za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wahakikishe wanakagua miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye maeneo yao na wajiridhishe kama inalingana na thamani halisi ya kiasi cha fedha kilichotumika.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Ametoa maagizo hayo leo (Jumamosi, Februari 16, 2019) wakati akizungumza na viongozi wa CCM, wabunge pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kigoma kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya CCM ya mkoa wa Kigoma.

Amesema iwapo viongozi hao hawataridhishwa na utekelezwaji wa mradi husika wasisite kuchukua hatua kwa kutoa taarifa katika ngazi huzika, lengo ni kuhakikisha miradi yote inakuwa na ubora na inalingana na thamani ya fedha iliyotolewa.

CCM ni chama imara chenye mipango inayotekelezeka na kilicholenga kuwaletea wananchi maendeleo na kushirikiana nao katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili na ndicho chama pekee chenye kuleta matumaini kwa Watanzania wote.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa CCM mkoa wa Kigoma amesema ni muhimu kwa viongozi hao kujiridhisha na muenendo wa utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo yao zikiwemo za afya, maji, elimu na kilimo.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewasisitiza wanachama na wapenzi wa CCM wasome katiba ya chama na kuzielewa kanuni, taratibu na sera ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Akisisitiza jambo hilo Waziri Mkuu amegawa nakala za katiba ya CCM kwa viongozi hao. 

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga alisoma taarifa ya mkoa huo, ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu linaloendelea kwenye mkoa huo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2018 jumla ya wahamiaji haramu zaidi ya 4,135 walikamatwa kwenye msako uliofanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
 

HABARI ZAIDI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita