Jumanne , 1st Nov , 2022

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa wanne wa ujangili  ambapo pia wamekutwa na vitu mbalimbali ikiwemo vipande viwili vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 33 pamoja na Nyamapori ya mnyama Pofu

Kamanda wa Jeshi la Polisi  mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amesema jithada hizo za kukamata majangili ni kutokana na msako wa jeshi hilo kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya taifa ya Ruaha

Kwa upande wake Kamanda wa uhifadhi nyanda za juu Kusini Joas Makwati amesema  meno hayo ya tembo ni ya muda mrefu na yalikuwa yamehifadhiwa na majangili hayo  kwa ajili ya kutafuta wateja 

Katika hatua nyingine jeshi hilo limefanikiwa kupata silaha 13 ikiwa ni mafanikio ya zoezi la kusalimisha silaha  lilioendeshwa katika maeneo mbalimbali