'Maji yamenifika shingoni' - Meya DSM

Jumatatu , 6th Jan , 2020

Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, amesema kwa sasa yuko hatarini kupoteza nafasi yake ya Umeya wa Jiji hilo, baada ya kuundiwa kamati maalumu ya uchunguzi na Mkuu wa Mkoa huo kufuatia uwepo wa malalamiko dhidi yake.

Akizungumza leo Januari 6, 2020 na EATV na EA Radio Digital, Meya Mwita amesema kwa asilimia kubwa ya tuhuma anazotuhumiwa si za kweli, huku akitoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kumuombea.

"Ni kweli Umeya wangu sasa unapimwa ikiwa imebaki miezi 3 kabla hatujavunja Baraza la Madiwani, na hivi karibuni nimeanza kupata wakati mgumu kwenye kiti changu, naomba Masheikh na viongozi wengine wa Dini waniombee" amesema Isaya Mwita.

Aidha ameongeza kuwa "Kiukweli sasa maji kwangu yapo shingoni, mbele sioni wala nyuma sioni ila naamini Mwenyezi Mungu atasimama na mimi" ameongeza Mwita.