Akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam leo, Disemba 2, 2025, Rais Samia alisema, “Tanzania haina dini, bali Watanzania tuna dini. Hakuna dini yenye mamlaka ya kuongoza nchi au kutoa matamko kwa niaba ya wengine.”
Ameeleza kuwa ndani ya muda wake madarakani, matamko manane yametolewa na TEC, lakini baadhi ya viongozi wa TEC wenyewe wameyapinga, jambo linalodhihirisha mgawanyiko wa kimtazamo hata ndani ya taasisi hizo.
Amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuongozwa kwa misingi ya katiba, mshikamano na amani, si kwa misingi ya matamko ya kidini. “Ubora wa dini upo moyoni, na kila mtu anawajibika mbele ya Mungu, si kwa matamko ya mtu mmoja,” aliongeza.



