
David Cleopa Msuya, Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, enzi za uhai wake
Rais Samia amesema kwamba David Cleopa Msuya, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu ndani na nje ya nchi ikiwemo Hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete, hospitali ya Mzena na London nchini Uingereza.
"Ninatoa pole kwa familia ndugu jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba mkubwa kwa Taifa, ninatangaza siku 7 za maombolezo na bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia tarehe 7 hadi tarehe 13," amesema Rais Samia