Makonda adai CHADEMA hawamtaki Meya Jacob

Jumatano , 1st Jul , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amesema aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob alikuwa akijitapa kwamba anaongoza Manispaa hiyo kisasa, na kumbe anayo makandokando mengi yaliyopelekea hata chama chake kumuondoa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Julai 1, 2020, wakati akiendelea na ziara yake ya kukabidhi miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa Chama cha Mapinduzi, huku akiwataka wananchi kuchagua watu sahihi na siyo kuangalia miili mikubwa.

"Sasa hapa alikuwepo mtu mmoja anatamba kwamba anaongoza Manispaa ya Ubungo kwa aina yake, wakati mwingine hii miili mikubwa muwe mnaiangalia mingine imejaa upepo tu, sasa bahati mbaya kumbe ana makandokando kibao, ameshindwa hata kumaliza Umeya wake na CHADEMA wenyewwe wameshindwa kumvumilia wamemuondoa wamegundua kwamba hamna kitu na Kata yake tangu awe Diwani hajawahi kuwa na Sekondari" amesema Makonda.